Posts

Showing posts from March, 2017

SABABU ZA MATAJIRI KURUDIA NGUO ZILE ZILE.

Kila siku tunafanya maamuzi mengi: unawaza niamke kutoka kitandani ama niendelee kulala kidogo, Ni muda gani niende kazini ama shuleni?, Leo nifanye mazoezi? na kama ndivyo, ni muda gani?, Nitakula chakula gani jioni? niendelee kufanya kazi au niende nyumbani? na mengineyo mengi Kuna vitu vingi sana tunavyopaswa kuviamua kila siku. Maamuzi mengine huwa ni ya manufaa, lakini mengi huwa ni yenye manufaa kidogo au yasiyo na manufaa kabisa. Kwa bahati mbaya, tafiti zimeonyesha kuwa sisi kama binadamu, uwezo wetu wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi na yenye manufaa una ukomo. Hii inamaana kuwa kile unachokiamua mapema asubuhi, huwa na nguvu kuliko kile unachokiamua baada ya ubongo wako kuwa umeshachoka. Hali hii hujulikana kama maamuzi kulingana na uchovu, ni hali ya kisaikolojia ambayo hupelekea ufanywaji wa maamuzi kwa muda uliopo kupunguza ufanyaji wa maamuzi kwa wakati ujao. John Tierney, mwandishi wa kitabu cha Willpower’ kilichouzwa sana na ‘The New York Times’ anasema, “Kufanya...

Ingiza pesa kupitia youtube

Jinsi ya kuwa na akaunti ya kibiashara ya Youtube #Maujanja 0 BY Nkya Henry .post-header Youtube ni mtandao ambao kila leo unazidi kuwa maarufu na kuzidi kuwa na mashabiki wengi. Tumeona watu mbalimbali wakiwa na chaneli zao binafsi huku wakiwa na uwezo wa kuweka video kwenye Youtube na watu kuangalia video kupitia wao. Je, unajua waliwezaje kufanikisha hilo? Mtu yeyote anaweza kuwa na Youtube chaneli yake binafsi hivyo kuweza kuweka video mbalimbali na watu kuweza kuona hivyo kujulikana na hata kulipwa kutokana na idadi ya watu wanaotazama video zako (views). Jambo la msingi na muhimu kuzingatia ni kuwa na barua pepe na kama hauna basi ni muhimu kuwa nayo. Hatua za kufuata wakati wa kutengeneza akaunti kwenye Youtube chaneli. 1. Tembelea tovuti ya Youtube. Upande wa kulia juu una sehemu mbili; kama hauna barua pepe au kama tayari una barua pepe ya Gmail unabonyeza “Sign in”. 2. Jaza sehemu zote kutengeneza barua pepe kama hauna ila kama tayari una barua pepe basi bonyeza “...

AKILI MOJA INAYOKIDHI AKILI ZOTE

*TIME & BUSINESS COACH* *Title: ONE MIND FITS ALL/ AKILI MOJA INAYOKIDHI(AKILI) ZOTE* ✳ *1 WAKORINTHO 2:16* 💯Akili ya mwanadamu inabadilika kama kinyonga kutokana na mabadiliko ya mazingira, kama ikitokea akili yako isipo badilika kulingana na mazingira Fulani mtu huyu anakuwa maskini tu. Akili uliyoishi nayo Arusha kwa muda wa  miaka 10(isiyokuwa na mafanikio) ikatokea ukatoka nje ya eneo hili ukaenda mahali pengine tena ukatumia akili ile ile uliyokuwa unaishi nayo Arusha huwezi kutoka kimaisha, kwa mfano akilli hiyo uliyo ishi nayo Arusha ukaenda ukaishi nayo Mwanza haitakufikisha mbali kimaisha utaona kuna vitu havifanyi kazi, utateseka sana. Ili akili yako ibadilike ufikapo Mwanza lazima ujue hao watu wanaishije, wanakulaje pamoja na mazingira yao yako vipi n.k . UKIWA SEHEMU MPYA, MAZINGIRA MAPYA NA UNATUMIA AKILI YA ZAMANI HUWEZI FANIKIWA KIMAISHA. ✅Akili isipotaka kubadilika hauwezi kuelewa kitu, akili ikikataa kufanya jambo fulani kuna mambo mengi huwezi faniki...

Mgunduzi wa facebook:Jifunze kupitia yeye.

Image
Pombe ilikuwa imemwingia kichwani kiasi flani na kumfanya ajiskie kuwa ni jasiri kwa namna moja ama nyingine, aliamua kunyanyuka  na kusogeleaa chumba kingine ambacho ndani yake kuliku wa kuna tukio la sherehe lililokuwa likiendelea, tukio la kuchagua baadhi ya wanafunzi wa chuoni pale ili wawez e kufanyiwa mchujo wa kuweza kujiunga katika clu b hiyo iliyokuwa ikifanya tukio lile. Eduardo Saverin  mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu kile kiichwato Harvard aliamua kuingia ndani ya chumba kile kilichokuwa kikiogofya kwa wingi wa watu kiasi kwamba alihisi kuishiwa ujasiri na kushindwa aanzie wapi ndani mle, aliangaza macho huku na kule na kuona meza karibu na alipokuwa amesimama, ni meza ambayo ilikuwa imekaliwa na watu wanne ambao aliangaza na kumwona mmoja wao akiwa amevalia mavazi yaliyomtambulisha kuwa yeye ni mwanachama wa club ile, aliamua kupiga moyo konde na kusogelea meza ile ili aweze kuongea na yule mwanachama ili kusudi na yeye apate mwaliko wa kuchaguliwa k...

Fahamu uwekezaji kwenye HISA.

https://m.youtube.com/watch?a=&v=lDIZRGm4_Ok&feature=youtu.be

Operation mole cricket

Operation Mole Cricket ni kampeni iliyofanywa na Israel dhidi ya Syria kuharibu Mizinga ya kutungulia ndege iliyo karibu na mpaka wa Israel pia ndani ya Syria.Hii ni operation ya kwanza ya kijeshi katika historia ambayo ilihusisha jeshi la anga lenye vifaa na teknolojia ya magharibi kuharibu kabisa mizinga yenye makombora ya kudungulia ndege yaliyotengenezwa na Umoja wa Kisovieti(USSR). Pia ni moja ya mapambano makubwa kabisa ya anga tangu vita ya pili ya Dunia na makubwa tangu yale ya vita vya Korea. Jeshi la anga la Israel lilianza kubuni na kutengeneza teknolojia na vifaa vya kuharibu mizinga ya kudungulia ndege tangu mwisho wa vita vya Yom Kippur.Mwaka 1980,joto la mvutano kati ya Israel na Syria juu ya Lebanon lilivyozidi kupamba kupanda iliwafanya Syria kuweka mizinga yenye Makombora ya kudungulia ndege katika eneo la Beqaa Valley. Juni 1982, Jeshi la Israel likavamia Lebanon huku mivutano yake na Syria ikiendelea, hii ilifanya Israel kuanzisha oparesheni ya kuharibu sehemu z...
Image
Mambo vipi karibu kwenye blog yangu mpya,hapa tutakuwa tunahabarishana habari mbali mbali za kujenga na zinazogusa jamii. Pia tutaongelea mambo mbali mbali yanayotokea duniani.