AKILI MOJA INAYOKIDHI AKILI ZOTE


*TIME & BUSINESS COACH*
*Title: ONE MIND FITS ALL/ AKILI MOJA INAYOKIDHI(AKILI) ZOTE*
✳ *1 WAKORINTHO 2:16*

💯Akili ya mwanadamu inabadilika kama kinyonga kutokana na mabadiliko ya mazingira, kama ikitokea akili yako isipo badilika kulingana na mazingira Fulani mtu huyu anakuwa maskini tu. Akili uliyoishi nayo Arusha kwa muda wa  miaka 10(isiyokuwa na mafanikio) ikatokea ukatoka nje ya eneo hili ukaenda mahali pengine tena ukatumia akili ile ile uliyokuwa unaishi nayo Arusha huwezi kutoka kimaisha, kwa mfano akilli hiyo uliyo ishi nayo Arusha ukaenda ukaishi nayo Mwanza haitakufikisha mbali kimaisha utaona kuna vitu havifanyi kazi, utateseka sana. Ili akili yako ibadilike ufikapo Mwanza lazima ujue hao watu wanaishije, wanakulaje pamoja na mazingira yao yako vipi n.k . UKIWA SEHEMU MPYA, MAZINGIRA MAPYA NA UNATUMIA AKILI YA ZAMANI HUWEZI FANIKIWA KIMAISHA.

✅Akili isipotaka kubadilika hauwezi kuelewa kitu, akili ikikataa kufanya jambo fulani kuna mambo mengi huwezi fanikiwa kwa mfano rahisi ulifanya biashara Fulani ukapata hasara naikatokea akili yako imeganda pale ulipo pata hasara, kumbe ile bishara ulipata hasara kwa sababu ya kipindi ambacho ulinunua bidhaa kwa bei nafuu harafu wewe ukawa unauza ghali wakati bidhaa hiyo inapatakana kwa wingi wakati huo ukapata hasara kwa hivyo basi usipotaka kubadili akili yako katoka mazingira ya zamani na kuingia mapya hutafakiwa.

✳Leo tunaangalia AKILI MOJA INAVYOKIDHI KWENYE MAENEO YA MAISHA YAKO (AKILI YA KRISTO). Akili ya Kristo inakidhi maeneo yote kwenye Biashara yako, kazini kwako, kwenye ndoa yako(Japo Yesu hakuwahi kuoa lakini Akili yake inakidhi kwenye ndoa), akili hii pia inakidhi mahitaji kwenye kilimo n.k Akili hii moja inakidhi kila sehemu ya maisha yako. Leo hii ukatumia akili yako moja uliyozaliwa nayo(Akili hasi) mwenyewe ikipata tu changamoto fulani inakwama utaona unaingiza hofu, uwoga,aibu n.k kwa lugha nyingine tunasema “Akili inaingiza upepo”

👉🏿 *Kuna aina mbili za watu duniani (Wakristo)*
1. Mkristo wa Dini tu (Mkristo jina tu)
2. Wana wa Mungu (Wafuasi wa Yesu Kristo-Yohana 1:12)

🔃 *Nyakati zilizopita tulifundisha madaraja manne ya  watu(There are four classes of people)*
*1. Upper Class*
*2. Middle Class*
*3. Low Class*
*4. Poor Class*

💯Nchi ya Marekani kwa mfano wao hawana Poor Class serikali imeimeza umaskini(inawalipia maskini) wao wana madaraja kuanzia namba 1-3, Kadhalika Tanzania hapa kwetu hatuna watu wanaoishi Upper class labda Bakhesa kwa maana bidhaa zake zipo kila mahali nchini na nje ya nchi(zinapatikana kwa bei nafuu). Tuna watu wengi wanaishi katika daraja la umaskini(Cha ajabu wasomi wengi wapo katika daraja hili kwa maana wanaishi “Public life”), daraja la chini na la kati.

✳Luka 4:18, Unapotaka kufanya biashara lazima uchague daraja ambalo unataka kuwa hudumia hao watu. Yesu Kristo alichagua daraja la maskini(Luka 4:18) cha kujiuliza hapa kwa nini Yesu Kristo aliamua kuchagua daraja la maskini? Alijua kabisa watu wengi ulimwenguni wanaishi kwenye daraja hili(Aliye na afya njema haitaji daktari wala dawa. Kama ilivyo wewe leo ukiamua biashara yako kuwa hudumia “upper class” na “middle class” siyo tu kwanza utapata wateja wachache lakini pia utawadharau “poor class” ambao wapo wengi duniani. Yesu Kristo aliiweka akili yake kwa maskini je wewe leo kwenye biashara yako umeweka akili yako wapi? Utambue ya kuwa dharau inakuja pale baada ya wewe kuitengeneza akili yako(kuiweka) ukisema huwezi ukawa hudumia maskini.

🏃🏿 *Maskini yeyote anahitaji vitu vifuatavyo kutoka kwa mfanyabiashara au mtu yeyote yule;*
*1. Kuaminiwa*
*2. Kuheshimiwa pamoja na*
*3. Kuhudumiwa*

✅ Ukimweshimu maskini vizuri utapata vitu vingi kutoka kwake tofauti na hapo huwezi kufanya chochote. Ukitazama Wachina leo wanatengeneza tu bidhaa ambazo zinatumika na Waafrika, waliamua kutuamini, kutuhudumia na kututendea haki kulingana na ghali halisi ya mazingira yetu. Kama tulivyofundisha wiki iliyopita “One-way mind” utatakiwa kuwaheshimu watu wa eneo fulani kulingana na daraja ulilopo wewe lakini unapoanza kidogo kidogo na baadae ukawa na biashara kubwa lazima utakumbuka ulipotoka na kuwahudumia watu wote “Two ways mind”.

🔃 Tengeneza akili yako kufanya kazi ya Adam (Mwanzo 2:15) na ya Yesu Kristo(Mathayo 1:21, 6:33). Biblia inasema Mungu atabariki kazi ya MIKONO YAKO (Ukifanya kazi ya mikono miwili-Kazi ya Adam). Vile vile Mungu amesema atabariki pia kazi ya MKONO WAKO (Kazi ya Yesu Kristo), Ayubu 1:9-10, Kumbu Kumbu la torati 28:12, 1:1-13. Hata kama umeajiriwa au una biashara yako au shamba utambue ya kuwa Baraka zote duniani zipo kwenye kazi ya Adam na Yesu.

✅Ukiona umefanya kazi muda mrefu pasipo mafanikio yeyote na hakuna Baraka yeyote ile ujue ya kuwa unavuna ulichopanda. Kama ni shule utavuna (Ukipata elimu utaenda kuomba kazi ili ulipwe mshahara) Kumbuka Fomula yetu Seed-Time-Harvest Mwanzo 8:22, Kwa maana bila kupanda mbegu huwezi fanikiwa maishani Mathayo 6:33, Kutoka 23:23-25, Ayubu 36:11, Isaya 3:10.
Kwa hivyo basi kama hujapanda mbegu kwa ajiri ya hiyo biashara au huduma utasubiri chakula cha msaada. Na ukumbuke ya kuwa ukiwa unafanya kazi isiyo ya kwako ujue huna tofauti na kichaa! Tunawashauri baadhi ya watu wakapimwe akili kwa maana kuna vitu wanafanya hata vichaa nao wanafanya vivyo hivyo! Tunasema AKILI YA YESU INAKIDHI MAHITAJI YOTE, Utajazwa hekima, maneno na matendo Ijulikane kuwa hata kichaa ana akili lakini hana HEKIMA wala MATENDO MAZURI,Ukitaka kujua kichaa ana akili utaona anakimbia moto hata barabarani anavuka kama watu wengine! *Jiulize leo unatofauti gani na kichaa?*

🙇🏾 1 Nyakati 12:32- Akili yako lazima isome alama za nyakati na mazingira ambayo yamekufanya uwe leo hii jinsi ulivyo na uyabadilishe haraka iwezekanavyo.

*HITIMISHO*
*Mtu anapo badilika kulinga na mazingira siku zote anafanya vizuri maishani, ukiona haufanikiwi tambua akili yako imeingiza upepo (imeingiza hofu, uwoga, aibu) Akili nyingi za maskini zimeingiza upepo na si oxygen kama watu wengi wanavyojua. Lazima utambue aina ya akili unayoitumia kwa mazingira yapi.*

Unaswali/Maoni/Mapendekezo komenti hapo chini au Una ushuhuda usisite kutuandikia!

Comments

Popular posts from this blog

Operation mole cricket